Home BURUDANI Msala wa DaBaby na Watetezi wa Haki za Mashoga.

Msala wa DaBaby na Watetezi wa Haki za Mashoga.

80
0

Siku ya Jumapili ya tarehe 26 ilisambaa video ya shabiki kumrushia kitatu Mwanamuziki Jonathan Lyndale Kirk almaarufu kama DaBaby. Baada ya hapo watetezi na wahusika kamili kutoka kwenye umoja wao wa LGBTQ wakaanza kuja juu na kumsema vibaya Dababy.

Makinipoint imejaribu kuchunguza nini hasa ilikuwa sababu hadi watu kams Madona na Elton John kumchukia ghafla Mwanamuziki huyu mzaliwa wa Ohio nchini Marekani.

Show ilipoanza huko Rolling Loud mjini Miami siku ya Jumapili, Dababy alimpandisha jukwaani Mwanamuziki Tory Lanez ambaye kesi yake ya kumshambulia mwanadada/mwanamuziki Megan Thee Stallion inafukuta. Lanez anashutumiwa kumpiga risasi ya Mguu Mwanadada Megan kwenye PoolParty ya Kylie Jenner. Nikusimulie kidogo, Lanez alikuwa kwenye gari na rafiki zake pamoja na mwanadada Megan, kwa muda walionekana wanagombana hivyo Megan kuondoa kesi akaamua kushuka kwenye gari na kuwaacha midume ikigombana yenyewe kwenye gari. Ghafla ulisikika mlio wa bastola na kumdhuru Megan mguuni. Taarifa ambayo ilisambaa haraka mtandaoni na kwa jeshi la Polisi ni kwamba Megan alijikata chupa na sio risasi, Megan alipoulizwa alisema aliogopa kutengeneza msala kwa Lanez hivyo akadanganya ni chupa japo uhalisia ni kwamba alipigwa risasi na anadai aliyemshambulia ni Lanez.
Japo Lanez hakuwa na sababu ya kumshambulia Megan, nadhani uchunguzi unaendelea hadi leo hii.

Tuje kwa Dababy, baada ya kumpandisha Tory Lanez jukwaani, aliimba wimbo aliomshirikisha Megan The Stallion unaoitwa “Cry Baby”. Hii ilianza kuwakera baadhi ya mashabiki kuwa kwanini ampandishe Lanez na kuimba wimbo aliowahi kumshirikisha Megan ilhali Megan na Lanez wanakesi nzito na kutopatana.

Shida kubwa inaendelea
Dababy akiwa kwenye show akasema “Kama umekuja humu ndani na hauna HIV wala ugonjwa wowote wa ngono unaoweza kuua ndani ya wiki tatu basi washa taa ya simu na umulike juuuu,
Kina dada kama *** yako inanukia kama maji (akimaanisha haitoi harufu) basi washa taa ya simu yako na umulike,
Masela, kama haujawahi kunyonya ** ya mwanaume mwenzako basi washa tochi ya simu yako na umulike juuuu.

Hawakumchelewesha walioipinga hii kauli na shabiki papohapo akamshambulia kwa Kumpiga kiatu.

Watumiaji wa twitter ndio walikuwa number moja katika kumshambulia Dababy kuwa hajawatendea haki MASHOGA. Kauli yake hii inaashiria kuwa hasupport hali hii wala hatakati zozote zinazotetea watu wa aina hii.
Dababy alijaribu kuuzima moto kwa kusema yale yalikuwa maneno ya mzaha kwa watu waliofika kwenye show yake na hata hivyo alitegemea wagonjwa HIV ndio wataumizwa zaidi kuliko Mashoga.

Watu hawajapoa mtandaoni wanamsema hadi sasa.

Madhara ni makubwa, kuna baadhi ya Matamasha wameshaanza kumfuta mwanamuziki huyo huku baadhi ya wasanii na watu maarufu wakiwa wanamsema vibaya Dababy kwa kunyanyapaa Mashoga.

Usishangae, hili si jambo la kawaida kwa nchi za Afrika. Ila ulaya na America wanajali sana kuhusu Mashoga.

Baadhi wamemtetea Dababy akiwemo mwanamuziki T.i.

Nafupisha maneno ya T.I
Anasema kumshambulia Dababy namna hii ni ukatili na unyanyasaji mkubwa. Sisi kama wasanii na wanaharakati tulihakikisha hakuna mtu anaingilia au kuwahukumu vibaya Mashoga. Kwanini Mashoga wanakuwa kipaumbele katika kuturudisha nyuma sisi tusioamini katika njia zao?. Je kosa ni kutoamini tu katika Mashoga? hii ni kawaida kwa mtu ambaye si wa aina hii.
Hayo ndo maneno ya T.I

Naye Boosie alitumia instagram yake kusema huu ni uonevu kwa Dababy. Mbona Lil Nas X ni shoga na alisema anatafuta show moja apande jukwaani uchi ili kujionyesha kuwa yeye ni wa aina gani?
Naapa kama Lil Nas X atapanda jukwaani uchi, nitakuwa number moja kati ya watu watakaomtandika mangumi na kumsukumia nje kwakuwa atakuwa amekosea ki maadili. Tuna watoto na sio lazima tuwaonyeshe ushoga ili na wao wawe mashoga, acheni kila mtu aishi kwa njia zake na tusilazimishane mifumo ya maisha.

Hayo ndiyo tuliyokuletea siku ya leo kuhusu Mwanamuziki Dababy

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here