Home BURUDANI Wimbo wa Kanye West “Nah Nah Nah” na Remix Aliyowashirikisha DaBaby na...

Wimbo wa Kanye West “Nah Nah Nah” na Remix Aliyowashirikisha DaBaby na 2 Chainz, Zapotea Ghafla Mitandaoni.

50
0

Wimbo bora wa mwaka 2020 uliofanywa na mwanamuziki Kanye West na baadae kufanya remix na wanamuziki Dababy pamoja na 2 Chainz zimefutwa mtandaoni ghafla wakati ambao raia wengi wanasubiri album mpya ya Kanye- DONDA
Wimbo huo ulikuwa unapatikana officialy kwenye majukwaa ya Spotify, Apple Music na Tidal lakini kwa sasa haupo.

Baadhi ya watu wamehisi labda huenda hii ni kutokana na Ukinzani kati ya DaBaby na watu wanaotetea LGBTQ Ambao wamemjia juu DaBaby kutokana na kauli yake ambayo imeonekana haijengi afya nzuri kati yake na watu wa aina hiyo.

Msala wa DaBaby na Watetezi wa Haki za Mashoga.


Dababy aliomba msamaha mara kadhaa lakini haikusaidia, kwani amefutwa kwenye matamasha mengi na pia ameingia hasara kubwa baada ya baadhi ya mikataba yake kufutwa kutonana na maneno yake hayo kwa LGBTQ.

Dababy Aomba Msamaha kwa Mara Nyingine


Upande wa Kanye West na Album ya DONDA, album hii ilitakiwa kutoka tarehe 23 July ikaahirishwa hadi tarehe 6 Agosti, bahati mbaya ilishindwa kutoka na hiyo imepelekwa mbele hadi tarehe 13 au 15 kama wanavyosema iTunes store na Apple Music.

Album ya Kanye West “DONDA” Yaahirishwa Hadi August 6

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here