Home HABARI MPYA VIDEO 2: Tunaomba Wakazi wa Lindi wawe kipaumbele wa Mradi wa GESI...

VIDEO 2: Tunaomba Wakazi wa Lindi wawe kipaumbele wa Mradi wa GESI Likong’o

75
0

Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Hamida Abdallah amewaomba wawekezaji, serikali na uongozi wa Mkoa wa Lindi, kutoa nafasi za kipaumbele kwa wakazi wa Lindi pale mradi wa kuchakata Gesi asilia utakapoanza kufanya kazi za awali.

Akizungumza katika ziara ya kutazama mradi huo iliyofanywa na waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani, Hamida amesema kuwa kiuhalisia mradi huu utapokea watu wengi na wafanyakazi wengi (binafsi na wa kuajiriwa) lakini amewataka wanalindi kuchangamkia fursa na pia uongozi wa mkoa huo kuwaweka mstari wa mbele pale zitakapotokea nafasi za ajira.

Aidha, kutokana na kampuni zilizowekeza katika mradi huo yani SHELL na EQUINOR kutokuwa na ofisi mjini hapo. Amewaomba wawekezaji hao kushirikiana naye pamoja ili aweze kuwasaidia kupata ardhi kupitia baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here