Home BURUDANI KUMBUKIZI YA GEEZ MABOVU ,MBWA MCHAFU WA KUSINI | 11 NOV 2021

KUMBUKIZI YA GEEZ MABOVU ,MBWA MCHAFU WA KUSINI | 11 NOV 2021

21
0

*Sio GEEZ MABOVU ni AHMED A. UPETE!!??*

Kumekucha,
Mapema tu napata taarifa kwa Geez Mabovu kaifariki dunia.
Nachukua laptop af naingia kwny file la miziki ya Geez Mabovu.
Natazama nyimbo zake nyingi nilizonazo naanza KU… zinacheza!!Zinachezaje !?
Tangia lini maiti ikacheza, tena ina Rap mistari ya kigangwe Ile mnaita Gansta Rap..Naaani anasema Geez kafa?
Geez bado yupo hai akiishi nasi masela wake wa kweli masela wa ghetto.

Skiliza mtoto wa kiume af niambie huyo mtu anakufaje?
Geez akiwa na Mau anakwambia Am alive, na huyo ndio Geez Mabovu, MwanaMadharau Mbwa Mchafu wa Kusini.

Wengi wameweka picha af wanasema r.i.p Geez??
huyo ni Ahmed Ally Utepe sio Geez.
Geez ni Geez mwana wa Mabovu mtoto Dolly South.

Geez sio picha, Geez sio Mwili wala Sio Ahmed.

Geez ni tungo, Geez ni michano, Midondoko, Hisia, Style, Geez ni Hip Hop.Ndio.

Hauwezi kuua tungo za Geez asilani na humo kwa Tungo Ndimo Uhai wa Geez ulipo na utaendelea kuwepo milele.

Nyimbo za Hip Hop  haziendi na wakati kama kiduku basi Geez ataishi nasi siku zote za maisha yetu.

Waliochagua ujinga walishajifia kitambo, wengine walikufa hata kabla kuifariki dunia.
kafa Mr.Nice na takeu yake, kafa Top C na ulofa wake, kafa Mr.Paul na buzi lake, kafa Farida na pesa zake.

Wengine walijitahidi angalau wakazikwa na nyimbo zao.

Sisi kwenye ukanda huu wa Hip Hop tutaishi Milele.

Pumzika kwa amani Ahmed, Ishi Milele Geez Mabovu🙏🏿🙏🏿

Imeandaliwa na Iddy Mwanaharamu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here