Home HABARI MPYA VIDEO: Tutumie Mbegu Asilia kwa Afya Zetu Pia Zinavumilia Mabadiliko ya Hali...

VIDEO: Tutumie Mbegu Asilia kwa Afya Zetu Pia Zinavumilia Mabadiliko ya Hali ya Hewa “Afisa Miradi SWISSAID”

43
0

Katika kuhakikisha afya za watanzania zipo salama, Shirika la misaada kutoka nchini Uswisi imefanya tamasha la kuonyesha na kuhamasisha matumizi bora ya vyakula na mbegu asilia. Mfumo huo wa kilimo asilia unajulikana kama KILIMO HAI, umedhamiria kukuza mbegu na kuvuna chakula kwa njia za asili bila kutumia kemikali zozote ambazo kwa sasa zimeonekana kuchagiza kwa kiasi kikubwa uwepo wa magonjwa yasiyoambukiza kama kansa na kisukari.

Afisa miradi SWISSAID TANZANIA, Veronica Masawe, amesema kwa sasa changamoto inayowakumba wakulima wengi ni kukosa elimu thabiti ya namna ya kuzalisha mazao asilia kwa wingi pamoja na njia sahihi ya kutunza bila kutumia kemikali.

Kwasasa, wakulima wengi wanahamasishwa kutumia mbegu zenye kemikali kwakuahidiwa kuwa zitakuwa salama mashambani na watavuna kwa wingi. Hivyo imesababisha mradi huu kupokea changamoto kwakuwa asilimia kubwa ya wazalishaji wanaamini katika kilimo cha kemikali.

SWISSAID imedhamiria kuwakomboa wakulima, walaji na mazingira kwa kuhamasisha kilimo hai. Kwani uchunguzi unaonyesha kilimo cha kemikali sio salama kwa walaji na mazingira kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here