Home HABARI MPYA VIDEO: Ujumbe wa Katibu wa ACT kwa Mama Samia Juu ya Tatizo...

VIDEO: Ujumbe wa Katibu wa ACT kwa Mama Samia Juu ya Tatizo la Mbolea Ruvuma

49
0

Katibu mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu kuwajali wakulima kwa kuweka Ruzuku ya mbolea kwani Licha ya wao kuwa tegemeo kubwa nchini, bado hali zao ni duni na wanashindwa kumudu gharama za viwatilifu.

Akizungumza na wananchi wa Songea Mkoani Ruvuma, Ado anasema, kitendo cha wakulima kutegemewa kwa asilimia kubwa na taifa ilhali wao wanajinunulia kila zana za kilimo bila msaada wa serikali ni sawa na kuwanyonya wakulima hao ambao wengi wao hali zao ni duni.

Pia, akiwa mkutanoni hapo, amewataka wenyeviti wa chama Cha ACT Wazalendo, kuwasilisha kero za wananchi katika vikao vya mashauri ya mkoa na sio kukaa kimya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here