Home HABARI MPYA VIDEO: Waziri Jafo Aonya Uharibifu wa Mazingira ya Bahari Mkoani Lindi na...

VIDEO: Waziri Jafo Aonya Uharibifu wa Mazingira ya Bahari Mkoani Lindi na Kilimo Holela

56
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais ,Muungano na Mazingira Selemani Jafo amewataka viongozi na wananchi wa Lindi kusimamia na kutunza mazingira ya bahari hasa kwa kupanda miti aina ya mikoko kwasababu hali ya bahari katika ukanda wa pwani inaonyesha kuto kuwa sawa kutokana na shughuli za uharibifu zinazofanywa na binadamu zinazosababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Akizungumza katika ziara yake mkoani Lindi, Waziri Jafo amesema ipo haja ya kutunza mazingira ya bahari, kwasababu athari ni kubwa endapo mambo muhimu hayatazingatiwa. “Hali ya bahari kwa mikoa ya pwani inaonyesha kutokuwa sawa, maji yanaongezeka na hata baadhi ya visiwa vimekuwa vikipotea kabisa” Waziri Jafo. Jafo anasisitiza ya kuwa, kati ya mikoa iliyopo hatarini kutokana na uharibifu wa mazingira ni pamoja na Lindi.

Akikumbuka mafuriko yaliyotokea wilayani kilwa mwaka 2019 anasema, ili kuepuka suala hilo ni vyema kwa wananchi kutunza mazingira na kudhibiti shughuli zote zinazosababisha uharibifu huo kama kilimo holela cha ukataji miti na uchomaji wa misitu katika kuandaa mashamba na ufugaji holela. Kwa sasa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imevalia njuga suala la mazingira na hii ni kutokana na kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Waziri Jafo anasisitiza suala la upandaji miti kwa wananchi na viongozi wote nchini ili kukomboa nchi katika majanga na mabadiliko yanayoleta athari kubwa kwa sasa. Mabadiliko hayo ni pamoja na kukosekana kwa mvua kwa wakati, hali ya joto nchini na Magonjwa ya Mlipuko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here