Home BURUDANI NAS AJIFANANISHA YEYE, BIGGIE NA JAYZ NI SAWA NA JCOLE, DRAKE NA...

NAS AJIFANANISHA YEYE, BIGGIE NA JAYZ NI SAWA NA JCOLE, DRAKE NA KENDRICK LAMAR, KWENYE ALBUM YAKE YA MAGIC

30
0

Kwa wasiofuatilia wanaweza kudhani Msuguano baina ya Nas na Jay Z unaendelea lakini nikuambie tu ya kuwa mtafaruk wao ulishakwisha zamani sana. Awali familia zao zilihusishwa kwenye michano na mwisho wakaamua kukaa chini na kuyajenga. Wakashirikishana kwenye nyimbo baadhi na hivi majuzi tumewaona kwenye album ya D J Khalid kibao cha Sorry not Sorry.

Siku kadhaa zilizopita, Nas ameachi album (LP ALBUM-MAGIC) yenye jumla ya Nyimbo 9. Kama wewe ni shabiki na mpenzi wa nyimbo za Hip Hop tena kwa wasanii wenye mafanikio ambao bado wanaiwakilisha mitaa vizuri kabisa, sidhani kama unaweza kuruhusu album ya Nas au wimbo wowote mpya kutoka kwa Mr I can ukupite. Hii ni kwasababu ya namna anavyotunga mashairi na jumbe zenye kuvutia na kufunza katika nyimbo zake.

Wimbo nambari 6 katika album hiyo unaitwa WU FOR THE CHILDREN, Naomba kwa leo nisihusianishe sana wimbo huu na harakati za kundi la Wu Tang Clan na msaada kwa watoto kuanzia mashairi na harakati zao binafsi hadi tukio la mwaka 1998 kwenye tuzo za Grammy (RIP Ol Dirty Bastard) hili nitalizungumzia siku nyingine au huko mbele naweza kutia nakshi nakshi kidogo.

Ndani ya Wu For the Children, Nas amezungumzia wasanii wachanga ambao wanaomba msaada kwa wasanii ambao wameshatoboa,
Pia amezungumza juu ya mashabiki zake wanaotaka muziki tofauti kutoka kwake
lakini pia amegusia kuhusu utofauti wa muziki wa sasa na wa zamani.

Na hapa ndipo aliposema

i shoulda had Grammys when Ol Dirty said WU For the Children.

Akimaanisha.
Nilipaswa kuwa na Grammy wakati Ol Dirty aliposema WU ni kwa watoto (Wu Tang Clan) nilisema nitatia nakshi kidogo. Marehemu Oldirty Bastard kutoka Kundi la Wu Tang Clan aliwahi kushangaza mashabiki katika tuzo za Grammy. Naomba nimnukuu kwa uchache, Alipanda jukwaani na kusema “leo nimeingia dukani na kununua nguo za gharama mno, nilidhani tutabeba ushindi..naomba mutambue Didy ni msanii bora lakini Wu Tang ni bora zaidi.Kumbukeni Wutang tunafanya kwaajili ya watoto, rap yetu inafundisha na kuonya…” WU TANG IS FOR THE CHILDREN. Yani ni kama Chid Benz alivyoshushwa na Kalapina jukwaani baada ya kuombwa Mike na Nikki Mbish kwa muda mrefu.

Lakini Oldirty aliongea maneno mazito kidogo. Tuachane na hili
Twende kwa Nas

Shoulda did that remix verse on gimme the loot for Biggie

Nas anaonyesha masikitiko kwa kusema, ni kheri angefanya remix ya Gimme the Loot (Wimbo wa Biggie) kwenye album yake ya Ready to die. Kumbuka Nas aliambiwa na Biggie afanye naye Remix lakini ilishindikana. Awali alitakiwa kufanya jambo kwenye album ya Ready to die lakini album ikatoka mapema kabla Nas hajafanya track hata moja

Anashusha mstari mwingine anasema ..
Me, Jay and Frank White is Like Cole, Drizzy and Kenny.

MIMI, JAY (JAY Z) na FRANK WHITE (BIGGIE😆 bwana Notorious aliwahi kujipa AKA ya Frank White, character ya Christopher Walken katika movie ya King of Newyork)

Sasa anajifananisha yeye, Jay z na Biggie ni kama COLE (J COLE) DRIZZY (DRAKE) na KENNY (KENDRICK LAMAR).

Je, Nas amepatia ulinganisho wa kizazi chake na huu wa wasanii wa sasa?.
Lakini hapa tunaona ni namna gani Nas anamkubali Jay Z licha ya misuguano waliyokuwa nayo hapo awali.
Lakini pia namna anavyoheshimu uwezo wa Biggie Notorious.
Lakini Kubwa kuliko, ni kuwapa heshima kubwa Mno Jcole, Drake na Kendrick Lamar.
Nadhani Nas amewabebesha mzigo mzito sana hawa vijana, kwasababu ya ubora wake yeye na wasanii aliowaunganisha yani JayZ na Biggie na kofia anayowavisha vijana hawa.
Nina imani kuna watu watafurahia mno kauli hii na kuna watu watakasirishwa kwa kutotajwa wasanii wanaowakubali, kwasababu ni ngumu mno kusema Jcole, Drake na Kendrick Lamar hawana uwezo mkubwa. Bali itawauma kwa wasanii wanaowakubali kutoa kutajwa.

Je tunahitaji List ya wasanii wanaopendwa na Nas kama Funga Mwaka????😂

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here