Home HABARI MPYA VIDEO: Tukiwa na Maono Sawa Tutapata Timu Moja ya Wilaya “DED MTAMA-LINDI”

VIDEO: Tukiwa na Maono Sawa Tutapata Timu Moja ya Wilaya “DED MTAMA-LINDI”

45
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi Bw. George Mbilinyi, amewataka wadau wa mpira na wananchi wa Mtama, kujadili kwa pamoja ili watambue ni namna gani wanaweza kuandaa timu moja ya mpira ambayo itawakilisha wilaya hiyo ya Mtama.

Akizungumza na wananchi katika sherehe ya ufunguzi wa tawi la Simba la Tunawakera, lililopo katika kata ya Nyengedi wilayani humo, Mbilinyi anasema, kwakuwa yeye ni mdau mkubwa wa mpira wa miguu baadhi ya watu wamekuwa wakitumia fursa hiyo kumshawishi kuanzisha timu za vijiji, kwa mantiki hii anaona ni muhimu kwa halmashauri nzima kuwa na timu moja ambayo itawakilisha wilaya.

Aidha, amewaasa wanachama wa tawi hilo kuandaa miradi mbalimbali itakayoweza kuwasaidia kujikimu kifedha ili nao wawe sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio ya timu ya Simba SC pale wanapohitajika huku akiwaahidi kushirikiana nao bega kwa bega kama mlezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here