Home HABARI MPYA Tuzingatie Zaidi Ufaulu wa Madaraja, ni Bora Kuliko Ufaulu Kitaifa “R.E.O LINDI”

Tuzingatie Zaidi Ufaulu wa Madaraja, ni Bora Kuliko Ufaulu Kitaifa “R.E.O LINDI”

37
0

Afisa elimu mkoa wa Lindi Venance Kayombo amewataka walimu na wataalamu wa masuala ya elimu mkoani humo kuwekeza nguvu kubwa katika kupandisha madaraja ya wanafunzi kwakua, Mkoa umekua ukishika nafasi nzuri kitaifa kwa sasa lakini bado madaraja ya wanafunzi yamekuwa ni madogo.

Akizungumza katika kikao cha Maabara ya elimu kilichofanyika Wilayani Ruangwa, Mkoani humo, Kayombo amesema ufaulu wa wanafunzi katika ngazi ya taifa umekua bora kwa asilimia 100 mkoani Lindi,hivyo uhakika wa watoto kufaulu ni mkubwa lakini ubora wa wanafunzi kamwe hauwezi kupimwa katika ufaulu wa shule kitaifa bali madaraja yao.

Anasisitiza, mikoa ya kusini yani Lindi na Mtwara imebahatika kuwa na fursa nzuri katika elimu, kwani kupitia zao la korosho wakulima wanatoa asilimia kadhaa ya fedha zao kwaajili ya kuendeleza sekta ya elimu, lakini pia kutokana na Mkoa wa Lindi kufanya vibaya hapo awali, walimu wake wanasifa ya kuelekezeka kwani kwasasa matokeo yamepanda kwa asilimia kubwa na mkoa unafanya vizuri.

Kupitia kikao hicho, Kayombo ameainisha changamoto 16 zinazoikabili sekta ya elimu mkoani Lindi ambapo suala la Wazazi kuwahadaa watoto wao wasifaulu mitihani kwa kigenzo cha kushindwa kuwasomesha limekuwa likishika hatam huku wanafanzi wakionekana kutofanya vizuri zaidi katika masomo ya Sayansi na Kiingereza.

Usimamizi duni wa viongozi mashuleni na ngazi ya kata inayosababisha kutomalizika kwa baadhi ya mada (walimu wakuu)

Aidha, Migogoro baina ya walimu wakuu na Maafisa elimu kata jambo linalotokea zaidi katika kuelimishana kuhusu utendaji wa kazi imekuwa ni changamoto pia huku changamoto ya usafiri ikiwa imetatuliwa kwa asilimia kubwa kwani hapo awali wasimamizi wa masuala ya elimu walikuwa wanashindwa kutembelea shule na kutazama maendeleo ya walimu na wanafunzi, Anaeleza Aisha Ngayaga ambaye ni Afisa elimu takwimu Wilaya ya Liwale

Mkakati uliopo sasa ni kuelekezana baina ya uongozi sekta ya elimu na walimu ambao hasa masomo yao hayajafanya vizuri ili kuzing’amua changamoto na kuzitatua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here